1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar es Salaam-Rais Karume wa Zanzibar awaalika waangalizi wa kimataifa kwa ajili ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

17 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFW9

Rais wa Zanzibar,Amani Abeid Karume amewaalika waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa katika uchaguzi wa mkuu visiwani humo uliopangwa kufanyika mwezi wa Oktoba mwaka huu.

Rais Karume aliyaeleza hayo katika taarifa ya serikali iliyotolewa muda mfupi baada ya kurejea ziarani nchini Finland ambako alikwenda kutafuta uungwaji mkono katika juhudi zake za kuinua uchumi wa Zanzibar.Amesema kuwa serikali yake haiwaogopi waangali wa uchaguzi wa kimataifa na kuwatolea wito waende Zanzibar kujionea wenyewe kiwango cha demokrasia katika visiwa hivyo.Hata hivyo Rais Karume amewataka waangalizi hao wa kimataifa watakaokwenda Zanzibar kuhakikisha wanafuata taratibu zote zitakazokuwa zimewekwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na waanze sasa kupeleka maombi yao kupitia Tume hiyo kwa ajili ya kuandaliwa vitambulisho na taarifa zinazohusu masuala ya usalama katika visiwa vyote vya Zanzibar na Pemba.