1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Makubaliano kumaliza mapigano nchini Burundi

16 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFD2

Rais wa Burundi ametia saini makubaliano ya kusimamisha mapigano na kundi pekee la waasi wa Kihutu linalopambana na serikali yake.Rais Domitien Ndayizeye na Agathon Rwasa,kiongozi wa FNL-kundi la waasi wa Kihutu wenye siasa kali,wametia saini makubaliano ya kumaliza mapigano,baada ya kukutana ana kwa ana kwa mara ya mwanzo mjini Dar es salaam,Tanzania.Pande hizo mbili katika kipindi cha mwezi mmoja ujao,zitakutana kwa majadiliano ya kupata suluhisho la mwisho la kuacha mapigano.Inakadiriwa kuwa watu 300,000 wameuawa nchini Burundi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 12.