1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar Es Salaam. Ghasia zazuka katika kampeni Zanzibar.

10 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CETM

Watu 18 wamejeruhiwa jana Jumapili, ikiwa ni pamoja na watu watatu ambao wamepata majeraha ya risasi wakati polisi katika kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania walipopambana na waandamanaji wa vyama vya upinzani , wamesema maafisa wa hospitali na wale wa vyama vya upinzani.

Ghasia hizo zilizuka baada ya polisi kuzuwia chama cha upinzani kufanya mkutano wake wa kampeni kabla ya uchaguzi mkuu wa bunge na rais uliopangwa kufanyika hapo oktoba 30.

Hilo ni tukio la hivi karibuni kabisa la ghasia katika kisiwa hicho chenye madaraka yake ya ndani, kabla ya uchaguzi.

Kiasi cha watu wawili wameuwawa na dazeni kadha wamejeruhiwa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi huko Zanzibar tangu mwaka jana.

Dr. Muchi Ahmed wa hospitali ya Al Rahma ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa hospitali hiyo imepokea watu 18 wakiwa na majeraha mbali mbali yaliyosababishwa na mabomu ya kutoa machozi, kipigo na watu watatu wamejeruhiwa kwa risasi.

Chama cha upinzani cha Civic United Front CUF, kimesema kuwa ghasia hizo zilizuka baada ya polisi walipoamuru chama hicho kuondoka katika eneo la wazi katika jimbo la Donge, kilometa 30 kaskazini ya mji mkongwe wa Zanzibar.