1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar Es Salaam. Bunduki na risasi zakamatwa bandarini.

27 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEh6

Maafisa wa Tanzania wamesema leo kuwa wamekamata silaha kadha zilizosafirishwa kutoka canada , miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Bunduki 17 pamoja na risasi 3,080 zilipatikana katika kontena ambalo halikuwa limeandikwa limebeba kitu gani na kukamatwa siku ya Jumatano na maafisa wa forodha mjini Dar Es Salaam.

Katika miezi ya hivi karibuni , taifa hilo la Afrika mashariki, ambalo limekuwa shina la uthabiti katika eneo lote, limekuwa likielezwa kuwa ni njia ya silaha kuingia katika eneo tete la maziwa makuu.