1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Dani Olmo ajiunga na Barcelona akitokea Leipzig

9 Agosti 2024

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atasaini mkataba na klabu hiyo ya Wakatalunya hadi 2030 katika mkataba wenye thamani ya awali ya yuro milioni 55.

https://p.dw.com/p/4jIpc
 Dani Olmo, RB Leipzig
Kiungo mchezaji wa Uhispania Dani Olmo amejiunga na Barcelona akitokea RB LeipzigPicha: Uwe Kraft/IMAGO

Kiungo mchezeshaji wa Uhispania Dani Olmo ameiaga rasmi RB Leipzig ya Ujerumani na kujiunga na klabu yake ya utotoni ya Barcelona.

Dani Olmo mwenyewe ameandika katika mtandao wake wa Instagram mapema Ijumaa akisema  "Asante sana kwa kunifanya kuwa sehemu ya kikosi cha RB Leipzig , daima nitawaweka moyoni mwangu."

Klabu ya Leipzig ilitangaza kuthibitisha kuwa nyota huyo anajiunga na Barcelona katika taarifa yao iliyosema "Asante sana kwa wakati mzuri tuliokuwa nawe pamoja na kwa pamoja tunakutakia kila lenye kheri katika hatua yako inayofuatia kwenye safari yako."

Soma zaidi.Leverkusen yaweka rekodi ya mwanzo bora wa msimu

Mshindi huyo wa Kombe la Ulaya alikuwa na kipengele cha kutolewa katika klabu ya Bundesliga lakini haikusababishwa na tarehe ya mwisho ya Julai.

Euro 2024
Dani Olmo ni mshindi wa Kombe la Ulaya akiwa na timu ya taifa ya UhispaniaPicha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atasaini mkataba na klabu hiyo ya Wakatalunya hadi 2030 katika mkataba wenye thamani ya awali ya yuro milioni 55.

Mkataba wake huko ulitarajiwa kukamilika hadi 2027. Ameondoka Leipzig akiwa ameshinda vikombe viwili vya Ujerumani baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Dinamo Zagreb mwaka 2020.