1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS:Mehlis yupo Syria kuwahoji maafisa juu ya kifo cha Hariri

12 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbv

Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafiq Hariri yupo nchini Syria kuwahoji maofisa nchini humo.

Kiongozi wa uchunguzi huo Detlev Mehlis anatarajiwa kukutana na maofisa wakuu wa usalama wa Syria waliokuwa wakifanya kazi Lebanon wakati mashambulio ya bomu yaliyosababisha kuwawa kwa Hariri yalipofanyika mjini Beirut.

Ziara hiyo imekuja miezi miwili baada ya Mehlis kutoa ombi lake la kutaka kuwahoji maofisa wa Syria.

Serikali ya Damascus imelaumiwa na wengi kwa mauji ya Hariri ambayo yalisababisha maandamano makubwa mjini Beirut ya kuitaka iyaondoshe majeshi yake nchini Lebanon.

Kufuatia hinikizo kutoka ndani ya Lebanon na kimataifa Syria iliyaondosha majeshi yake Lebanon baada ya kuikalia nchi hiyo kwa takriban miongo mitatu.