1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS : Umoja wa Mataifa yakutana na Syria

3 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQh

Kabla ya mkutano wa leo hii nchini Syria mjumbe wa Umoja wa Mataifa Terje Roed Larsen amesema ana matumaini juu ya matokeo ya mazungumzo na uogozi wa nchi hiyo.

Larsen anatazamiwa kukutana na Rais Bashar al Assad mjini Damascus kujadili ratiba ya kuondolewa kikamilifu kwa vikosi vya Syria nchini Lebanon.Syria imekuwa chini ya shinikizo zito la kimataifa kuondowa wanajeshi wake katika nchi jirani ya Lebanon kufuatia kuuwawa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafik Hariri ambapo wananchi wengi wa Lebanon wanailaumu Syria kuwa na mkono wake.

Mkutano wa viongozi wa pamoja kati ya Syria na Lebanon wiki ijayo utakamilisha ratiba kamili ya kuondolewa kwa vikosi hivyo ambapo Umoja wa Mataifa unataka ufanyike kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika hapo mwezi wa Mei.