1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR: Mkutano wa uchumi na biashara waanza nchini Segal

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtI

Mkutano juu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Marekani na Afrika umeanza leo mjini Dakar, Senegal. Mkutano huo unawajumulisha washiriki 1,000 wakiwemo mawaziri wa serikali mbalimbali barani Afrika.

Mazungumzo hayo, ambayo yanatarajiwa kuendelea hadi Jumatano, yalifunguliwa rasmi kwa hotuba za waziri wa biashara wa Senegal, Abdou Diop, waziri wa kilimo wa Marekani, Mike Johanns na rais wa Senegal, Abdoulaye Wade.

Mkutano huo unalenga kuyahimiza mataifa ya Afrika kuuza bidhaa zao kwa wingi nchini Marekani, licha ya sheria ngumu za Marekani kuruhusu bidhaa kutoka mataifa ya kigeni na swala tete la ruzuku inayotolewa na Marekani kwa wakulima wake kwa bidhaa kadhaa.