1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAGESTAN : Polisi watatu wauwawa katika mripuko

21 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiy

Gari lililotegwa mabomu kwenye jimbo la Dagestan nchini Russia karibu na Chechnya limeripuka na kuuwa polisi watatu na kujeruhi wengine wanne.

Shirika la habari la Interfax limeripoti kwamba gari hilo lilikokuwa limesheheni mabomu liliripuka wakati doria ya polisi ilipokuwa inapita pembeni mwake.Dagestan eneo lilioko kwenye bahari ya Caspian imekuwa katika msukosuko kutokana na umwagaji damu wa Chechnya tokea vita vya kutaka kujitenga kwa jimbo hili vilipozuka zaidi ya muongo mmoja uliopita.