1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wakishangilia makubaliano ya kihistoria.

24 Septemba 2016

Mwanasiasa wa mrengo wa kushoto Jeremy Corbyn amechaguliwa tena kuongoza chama cha Labour Uingereza Jumamosi (24.09.2016) na kuzima upinzani wa kutoka kwa wabunge wa chama chake kilichogawika.

https://p.dw.com/p/2QYdX
Jeremy Corbyn Parteisieg England
Picha: picture-alliance/dpa/D.Lawson

Wafuasi wake huko Liverpool kaskazini magharibi mwa England waliibuka kwa vifijo wakati Corbyn mwenye umri wa miaka 67 akipotangazwa kuwa mshindi kwa kijizolea asimilia 61.8 ya kura za wanachama na wafuasi wake na hiyo kumshinda kwa urahisi mpinzani wake mbunge Owen Smith.

Katika hotuba yake ya kukubali ushindi Corbyn amehimiza umoja na kuahidi kuanza upya baada ya kushutumiwa kwa maonevu na kuhofiwa kuzuka kwa utengano usiorekebishika kati ya wafuasi wa sera za mrengo wa kushoto na wale wa sera mrengo wa wastani ndani ya chama.Amesema "Wanafanana kwa mengi kuliko kile kinachowatafautisha.Kwa kadri ninavyohusika tuanze upya kuanzia leo na tuendelee na kazi inayotubidi kufanya kwa pamoja kama chama."

Corbyn ameongeza kiwango chake cha kura kutoka asilimia 59.5 alichopata wakati wa kuchaguliwa kwake awali mwaka jana wakati alipoipa kipau mbele agenda ya kupinga kubana matumizi na kupinga silaha za nyuklia katika siasa za Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kipindi cha kizazi kizima.

Pigo kwa wapinzani wake

Großbritannien Labour Partei Jeremy Corbyn Owen Smith
Jeremy Corbyn (kushoto) na mpinzani wake Owen Smith katika mdahalo.Picha: picture-alliance/dpa/N. Munns

Ushindi wake huo wa haja ni pigo kubwa kwa wabunge wa chama cha Labour ambao walimuasi baada ya kura ya Brexit Uingereza kujitowa Umoja wa Ulaya hapo mwezi wa Juni wengi wao walikuwa na msimamo wa wastani ambao walikuwa wakiamini kwamba msimamo wake wa kisoshalisti hautokubaliwa na wapiga kura wengi.

Corbyn alishutumiwa kwa kuendesha kampeni chapwa kwa Uingezeza kuendelea kubakia Umoja wa Ulaya na wengi hivi sasa wanahofu hawezi kutowa ushindani unaohitajika wakati chama cha Conservative cha Waziri Mkuu Theresa May kikijadili masharti ya kujitowa.

Corbyn anadai ameshajiisha watu wengi waliokuwa wameachwa nyuma na vyama vikuu vya kisiasa nchini Uingereza na kuzilinganisha juhudi zake na zile za mavuguvugu ya kupinga serikali yaliyozagaa barani kote Ulaya kama vile la Syriza nchini Ugiriki.

Tamaa ya kuingia madarakani

Großbritannien Jeremy Corbyn
Jeremy Corbyn .Picha: Getty Images/C. Furlong

Wanachama wa Labour hivi sasa wanafikia 650,000 wakiongezeka kutoka 200,000 miezi 18 iliopita kitu ambacho Corbyn anasema hatimae kitakiweka chama hicho madarakani.

Lakini wachambuzi wanaona kiko nyuma sana ya chama cha Conservative kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni na umashuhuri wa Corbyn uko chini kabisa.

Msemaji wa mambo ya ndani wa chama hicho Andy Burham amesema vita vya kuchoshana vya chama hicho lazima hivi sasa vikomeshwe na kumhimiza Corbyn kujenga uungaji mkono miongoni mwa wananchi na sio tu wafuasi wa chama.

Mwandishi : Mohamed Dahaman/AFP

Mhariri :  Bruce Amani