1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Comoro yakataa kuwapokea wahamiaji wa Mayotte

21 Aprili 2023

Visiwa vya Comoro vimeapa kutowapokea wahamiaji waliofurushwa katika kisiwa jirani cha Ufaransa cha Mayotte, katika operesheni iliyoibua mvutano wa kidiplomasia.

https://p.dw.com/p/4QPn1
Schiff mit 680 Tonnen Sprengstoff
Picha: AP

Maafisa katika kisiwa cha Mayotte wanatarajiwa kuanzisha operesheni kali mapema wiki ijayo ya kuwaondoa wahamiaji haramu ambao wameishi katika maeneo ya mabanda kisiwani humo.

Wale wasio na vibali watarejeshwa katika mojawapo ya visiwa vya Comoro cha Anjouan kilichoko kilometa takribani 70.

Msemaji wa serikali ya Comoro, Houmed Msaidie, amesema mipango ya kuwarejesha wahamiaji inakwenda kinyume na makubaliano baina ya nchi hizo mbili.

Awali, Comoro iliitolea wito Ufaransa kusimamisha operesehni hiyo iliyopitishwa na Rais Emmanuel Macron mnamo mwezi Februari. Mayotte na visiwa vitatu vinavyounda taifa la Comoro vilikuwa sehemu ya eneo la Ufaransa kufikia mwaka 1975.