1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo. Hali ya hatari yatangazwa kufuatia kifo cha waziri wa mambo ya kigeni.

13 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElF

Imetangazwa hari ya hatari nchini Sri Lanka kufuatia kuuwawa kwa waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo.

Lakshman Kadirgamar aliuwawa kwa kupigwa risasi Ijumaa jioni na mtu ambaye hakutambulika.

Taarifa zinasema kuwa waziri huyo wa mambo ya kigeni aliuwawa katika viwanja vya nyumbani yake katika mji mkuu Colombo.

Taarifa za kijeshi zinasema kuwa waasi wa Tamil Tigers nchini humo ndio wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kuuwawa kwa Kadirgamar.

Rice amesema kifo cha waziri huyo ni kitendo cha kigaidi ambacho Marekani inakishutumu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Canada nae pia ameshutumu mauaji hayo na kutoa rambi rambi zake kwa watu wote wa Sri Lanka.