1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE : Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ziarani Afrika

25 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9C

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amewasili barani Afrika kwa ziara ya siku tatu kukaguwa vikosi vya Ujerumani vilioko barani humo.

Ziara hiyo inamfikisha Djibouti,Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.Kituo cha kwanza cha ziara hiyo ya Jung ni Djibouti ambapo wanajeshi 350 wanapiga doria kwenye pwani ya Pembe ya Afrika kama sehemu ya operesheni ya kupiga vita ugaidi inayojulikana kama Enduring Freedom.

Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo anatazamiwa kuwa na mazungumzo na Rais Joseph Kabila na kiongozi wa upinzani Jean - Piere Bemba.