1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE : Fischer akiri makosa

27 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFao

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer amekiri hadharani kwamba alifanya makosa kwa kile kilichokuja kujulikana kuwa kisa cha visa.

Fischer ametowa taarifa hiyo kwenye mkutano wa chama chake cha Kijani mjini Cologne.Chama cha upinzani cha Christian Demokrat kimemtaka Fischer kujiuzulu kutokana na suala hilo. Chama hicho kimesema kuregezwa kwa taratibu za viza kulikoanzishwa na serikali katika miaka ya 1990 kumewanufaisha magenge ya uhalifu kuwaingiza nchini Ujerumani kwa magendo wahamiaji kutoka Ukraine na sehemu nyengine za Ulaya ya Mashariki.

Kansela Gerhrad Schroeder amekataa wito huo unaotolewa kila mara kumtaka waziri huyo wa mambo ya nje ajiuzulu.