1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Baba Mtakatifu atembelea hekalu la Wayahudi

20 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjO

Benedikt wa 16 ni Baba Mtakatifu wa pili anaejulikana kutembelea hekalu la Wayahudi.Papa Benedikt alitoa hotuba kwenye hekalu la mji wa Cologne nchini Ujerumani kwa muda wa dakika 10.Hekalu hilo limejengwa upya baada ya kuteketezwa na serikali ya Wanazi.Papa Benedikt wa 16 amelaani maangamizi ya Wayahudi na amesema Wakristo na Wayahudi wanapaswa kushirikiana ili kuhakikisha kuwa „itikadi kijinga yenye ubaguzi“ haitojitokeza tena.Mkuu wa jumuiya ya Wayahudi nchini Ujerumani,Paul Spiegel amesema kuwa amevutiwa na hotuba ya Baba Mtakatifu.Hapo awali Papa Benedikt wa 16 alikutana na Rais Horst Köhler wa Ujerumani katika mji mkuu wa zamani,Bonn.Leo jumamosi,Baba Mtakatifu atakutana na viongozi wa jumuiya ya kiislamu,iliyokuwa na Waturuki wengi.Vile vile atakutana na Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder na kiongozi wa chama cha kihafidhina cha upande wa upinzani,Bibi Angela Merkel.Papa Benedikt yupo Cologne kwa sherehe ya vijana wa kikatoliki waliotoka kila pembe ya dunia.Sherehe hiyo itakamilishwa kwa misa itakayoongozwa na Baba Mtakatifu siku ya jumapili.Zaidi ya waumini laki nane watahudhuria misa hiyo itakayosomwa katika uwanja wa Marienfeld,nje ya mji wa Cologne.