1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yawaadhibu maafisa 62 baada ya kuporomoka kwa jengo

21 Mei 2023

China imetoa onyo na adhabu nyingine kwa maafisa 62 baada ya kuporomoka kwa jengo la makazi katika mji wa Changsha mkoani Hunan na kuua watu 54 mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4RdI7
China | Einsturz eines Gebäudes in Changsha
Picha: CNS/AFP/Getty Images

Shirika la habari la taifa hilo, Xinhua limesema maafisa kadhaa na wakuu wa jiji walipewa onyo kali, akiwemo Zheng Jianxin, mkuu wa sasa wa Changsha ambaye alifukuzwa kazi.

China imechapisha ripoti ya uchunguzi iliyohusu kuporomoka kwa jengo hilo ikisema kulisababishwa na ujenzi usio zingatia utaratibu  na usio wa kawaida, huku viongozi wa eneo hilo wakishindwa kuzuia shughuli hizo za ujenzi na hatari zilizilizo jificha.

Ripoti ya mkasa huo ilisema watu 54 walikufa, wakiwemo wanafunzi 44 wa chuo, na raia wengine tisa wa kawaida, katika tukio lililosababisha hasara ya moja kwa moja ya dola za kimarekani milioni 13.1.