1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaonya dhidi ya kutanuka mzozo wa mashariki ya kati

30 Januari 2024

China imeonya leo dhidi ya kile imekitaja kuwa tabia ya kila upande kutaka kulipa kisasi katika mvutano wa eneo la Mashariki ya Kati, baada ya Marekani kusema itajibu shambulizi lililosababisha vifo vya wanajeshi wake.

https://p.dw.com/p/4bqGo
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang YiPicha: Sergio Lima/AFP

Washington inawatuhumu wanamgambo wenye mafungamano na Iran kuhusika na shambulizi hilo lakini serikali mjini Tehran imekanusha madai hayo. 

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya China imesemaimezisikia kauli za kila upande na kwamba ina matumaini mataifa hayo mawili yatajizuia kuutanua msuguano wa Mashariki ya Kati kwa kuepuka mwenendo wa kulipa kisasi.

Soma pia:China yaongeza shinikizo la kijeshi kwa Taiwan baada ya ziara ya maafisa wa marekani

Vifo vya wanajeshi hao wawatu wa Marekani -- ambavyo ni vya kwanza tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas -- vimeongeza mashaka ya kuchochea mzozo kwenye kanda hiyo licha ya Washington kusema "haitaki vita na Iran".