1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yamnyonga mwalimu aliyewapa sumu wanafunzi wake 25

14 Julai 2023

Mahakama moja nchini China imesema leo kuwa mwalimu wa shule ya chekechea aliyewapa sumu waanfunzi wake 25, na kumuuwa mmoja, amenyongwa.

https://p.dw.com/p/4TtiP
Symbolbild China Zensur
Picha: Wang Zhao/AFP/Getty Images

Taarifa ya mahakama ya mji wa Jiaozuo katika mkoa wa Henan imesema hukumu ya Wang Yun imetekelezwa jana Alhamisi.

Mwalimu huyo kike aliyekuwa na umri wa miaka 40, alihukumiwa kwa kuweka sumu kwenye uji wa watoto wa shule ya chekechekea ya Mengmeng mnamo Machi 27, 2019, kufuatia ugomvi na mwalimu mwenzake kuhusiana na usimamizi wa wanafunzi.

Wakati wanafunzi wengine walipona haraka, mmoja, alifariki kutokana na viungo kushindwa kufanya kazi baada ya miezi kumi ya matibabu.

Mwalimu huyo ambaye aliwacha masomo katika shule ya sekondari, awali alimpa mumewe sumu kama hiyo aliyonunua kwenye intaneti miaka miwili iliyopita lakini mumewe huyo alinusurika tukio hilo.