1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang afukuzwa kazi

26 Julai 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang amefukuzwa kazi na nafasi yake imechukuliwa na Wang Yi. Wang, ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa China.

https://p.dw.com/p/4UOad
Waziri wa mambo ya nje wa China- Qin Gang
Waziri wa mambo ya nje wa China aliyefukuzwa kazi - Qin GangPicha: Thomas Trutschel/photothek/picture alliance

Taarifa zinaeleza kuwa hakuna sababu zilizotolewa za kuondolewa Qin, lakini vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa Rais Xi Jinping alisaini amri ya rais kuchukua uamuzi huo.

Qin hajaonekana hadharani tangu Juni 25

Qin aliyeteuliwa Desemba mwaka 2022, hajaonekana hadharani tangu Juni 25, na pia hakuhudhuria mkutano wa kilele wa kimataifa wa wanadiplomasia uliofanyika nchini Indonesia. Baada ya hapo, wizara ya mambo ya nje ya China ilisema kutoonekana kwake kunatokana na matatizo ya kiafya.

Blinken anatarajia kufanya kazi vizuri na Wang

Wang ni kiongozi wa halmashauri ya masuala ya kidiplomasia ya Chama cha Kikoministi cha China. Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, amesema anatarajia kufanya kazi vizuri na Wang.