1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yajitetea kuhusu makubaliano ya biashara na Marekani

10 Februari 2022

China hii imeyapinga madai kwamba ilishindwa kuyasimamia makubaliano ya kibiashara na Marekani ya mwaka 2020 na badala yake imeitaka Washington kuiondolea mara moja kodi na vikwazo ilivyoviweka.

https://p.dw.com/p/46nsc
USA Präsident Biden trifft Chinas Präsident Xi Jinping
Picha: Huang Jingwen/Xinhua/picture alliance

Matamshi hayo yanatolewa wakati juzi Jumanne Marekani ikichapisha takwimu zilizoonyesha nakisi ya biashara na China ikiongezeka kwa shilingi bilioni 6 na kufikia jumla ya dola bilioni 34 mwezi Disemba mwaka jana.

Baada ya mzozo wa muda mrefu mataifa hayo mawili yalifikia makubaliano yaliyoitwa awamu ya kwanza, Januari 2020 ambapo Beijing iliahidi kuongeza manunuzi ya bidhaa na huduma za Marekani kwa angalau dola bilioni 200 kwa mwaka 2020 na 2021.

Hata hivyo baada ya makubaliano hayo kulishuhudiwa mvutano wa kibiashara yaliyosababisha aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na Xi Jinping wa China kuwekeana kodi za visasi za mabilioni ya dola.

Washington inalalama kwamba Beijing haisimamii ahadi zake kwenye makubaliano hayo huku takwimu hizo za Jumanne zikionyesha wazi upungufu huo.