1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China, baadhi ya nchi za Asia kufanya luteka ya kijeshi

12 Novemba 2023

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali nchini China, Xinhua limeripoti leo Jumapili kwamba, nchi hiyo itafanya luteka ya kijeshi ya pamoja na nchi tano za kusini Mashariki mwa Asia.

https://p.dw.com/p/4YiU5
Wanajeshi wa China wakiwa kwenye mazoezi
Wanajeshi wa China wakiwa kwenye mazoezi Picha: CFOTO/picture alliance

Luteka hiyo ya kijeshi itafanyika kuanzia katikati hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba.

Soma zaidi: Taiwan yatiwa wasiwasi na mazoezi ya kijeshi ya China

Mazoezi hayo ya kijeshi  yatafanyika katika mkoa wa Guangdong na yatahusiha vikosi vya Cambodia,Lao,Malaysia,Thailand na Vietnam.

Shirika la habari la Xinhua limesema pia kwamba mazoezi hayo yatajikita zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi na usalama wa baharini.