1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaifuta ziara ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa EU

5 Julai 2023

Umoja wa Ulaya umesema kuwa China imeifuta ziara ya mwanadiplomasia mkuu wa umoja huo Josep Borell iliyopangwa kuanza Julai 10.

https://p.dw.com/p/4TShm
Luxemburg | Josep Borrell Fontelles
Mwanadiplomasia mkuu wa umoja wa Ulaya Josep Borell Picha: Sierakowski/EUC/ROPI/picture alliance

Umoja wa Ulaya umesema kuwa China imeifuta ziara ya mwanadiplomasia mkuu wa umoja huo Josep Borelliliyopangwa kuanza Julai 10 katika wakati pande hizo mbili zinatofautiana pakubwa juu ya masuala muhimu ikiwemo biashara, haki za biandamu na vita nchini Ukraine.

Msemaji wa umoja huo Nabila Massarali amesema wamearifiwa na wenzao wa China kuwa ziara ya mkuu ya sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya mjini Beijing haitaweza kufanyika kwa tarehe zilizoainishwa hapo kabla bila ya kutoa sababu.

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wakutana Luxemburg

Wakati wa ziara hiyo Borell alikuwa amepangiwa kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nchi za nje wa China  Qin Gang na wanadiplomasaia wengine wa nchi hiyo kuhusu biashara, haki za binadamu na msimamo wa Beijing kuhusu vita vya Ukraine.

Kwa upande wake China imesema inathamini mahusiano kati yake na Umoja wa Ulaya na itatafuta muda mwafaka wa kumaribisha tena Borell kuitembelea nchi hiyo.