1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yafanya luteka ya kijeshi kuzunguka Taiwan

9 Januari 2023

China imesema imefanya luteka ya kijeshi kuzunguka kisiwa cha Taiwan jana Jumapili ikiwa ni mara ya pili kwa mazoezi ya aina hiyo kufanyika ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

https://p.dw.com/p/4Ltlj
Kirgistan | Chinesische Soldaten bei einer Übung
Picha: Vyacheslav Oseledko/AFP/Getty Images

Taarifa iliyotolewa na jeshi la ukombozi wa umma wa China, imesema vikosi vyake vilifanya mazoezi ya utayari kwa lengo la kupima uwezo wa kujibu vitendo vyovyote vya uchokozi kutoka nje na vikosi vya wanapigania uhuru wa Taiwan.

Luteka hiyo imefanyika katika wakati wanasiasa wa chama mshirika wa serikali ya mseto nchini Ujerumani, FDP, wanafanya ziara kwenye mji mkuu wa Taiwan, Taipei.

Ziara hiyo inayotajwa kuwa inalenga kuonesha shikamano na kisiwa cha Taiwan katikati mwa kitisho kinachoongeza kutoka Beijing, imekosolewa vikali na ubalozi wa China nchini Ujerumani.

China inakizingatia kisiwa cha Taiwan kinachojitawala kuwa sehemu ya himaya yake na imesema mara kadhaa inalenga kukirejesha chini ya milki yake hata kwa kutumia mabavu.