1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaamuru kufungwa ubalozi mdogo wa Marekani Chengdu

Sekione Kitojo
24 Julai 2020

Miongo minne baada  ya  Marekani kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia  na  China ya  kikomunist, uhusiano  huo kati ya  nchi hizo mbili  zenye uchumi  mkubwa duniani  uko  njia  panda.

https://p.dw.com/p/3frWB
China Chengdu | US Konsulat
Picha: Getty Images/AFP/G. Chai Hin

Hali ya wasi  wasi  imefikia kiwango kipya cha juu  katika  kile  wakati  wote kilichokuwa barabara iliyojaa mashimo na mawe, wakati  matarajio na  dhamira  ya  taifa hilo linaloinukia  kuwa  taifa  kubwa yakikinzana na yale  ya taifa  ambalo tayari ni taifa lenye  nguvu kama  Marekani. 

China Chengdu | US Konsulat
Ubalozi mdogo wa Marekani nchini China katika mji wa Chengdu ulioamuriwa kufungwa na serikali ya ChinaPicha: Getty Images/AFP/G. Chai Hin

China  imeamuru kufungwa  kwa  ubalozi  mdogo wa Marekani katika mji  wa  kusini mgharibi mwa  nchi  hiyo wa Chengdu jana  Ijumaa, ikiwa  ni ulipizaji  kisasi  wa  haraka  kutokana  na  kufungwa  kwa ubalozi  wake  mdogo  mjini  Houston.

Wiki  mbili  zilizopita, waziri wa mambo  ya  kigeni  wa  China Wang Yi alikuwa kijiuliza  iwapo  mahusiano  hayo yanaweza  kubakia kuwa katika njia ya kawaida. Siku  ya  Alhamis, waziri  wa  mambo  ya kigeni  wa  Marekani  Mike  Pompeo  alitoa  jibu. Alisema  muda umewadia  kubadilisha  mwelekeo.

"Dhana ya kale  ya  mahusiano  ya  kuifumbia macho  China haitawezekana," alisema  katika  hotuba  katika  maktaba  ya  rais Richard Nixon huko katika  eneo  la  kusini  mwa  Califonia. "Hatupaswi  kuendelea  nayo. Hatulazimiki  kuirejea."

Amri ya  kuufunga  ubalozi mdogo mjini  Chengdu, katika  jimbo  la kusini magharibi  mwa  China , kunaonekana kama jibu kwa mujibu wa  athari  na  kiwango, ikiendeleza utaratibu wa China  wa  jibu  la jino  kwa  jino kwa  hatua za  Marekani.

UK I Mike Pompeo in London
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike PompeoPicha: picture-alliance/AP/P. Summers

Athari ya hatua za Marekani kwa China

Msemaji  wa  wizara  ya mambo  ya  kigeni  ya  China Wang Wenbin alisema.

"Julai 21 Marekani  ilifanya  uchokozi kwa kudai ghafla  kuwa China ifunge ubalozi wake  mdogo mjini  Houston. hatua  hiyo ya Marekani  inakiuka sheria  za  kimataifa, misingi ya utaratibu wa  mahusiano ya kimataifa, na  masharti ya  makubaliano ya kibalozi kati ya China  na  Marekani. Hatua hiyo imeathiri  kwa kiasi kikubwa  uhusiano kati ya China  na  Marekani."

Ilikuwa  ziara  ya  Nixon  nchini  China   mwaka 1972, ikiwa  ni  ziara ya  kwanza  kufanywa  na  rais  wa  Marekani  tangu  wakomunisti waingie madarakani  mwaka  1949, iliweka kando kiasi utaratibu  wa vita  baridi  na  kusafisha  njia kwa  ajili  ya  kurejesha  mahusiano mwaka  1979.

Marekani  imekuwa  mshirika  wa  karibu  wa  kiongozi  wa  wakati huo Chiang Kai-shek  katika  vita  vikuu  vya  pili  vya  dunia na  kwa muda  wa  miongo  mitatu  iliitambua  Taiwan kama  serikali ya China  baada  ya  Chiang  kukimbilia  huko  wakati  alipopoteza mpambano wa  udhibiti  wa  China  bara  dhidi  ya  Wakomunist mwaka 1949.

Schließung des chinesischen Konsulats in Houston verfügt
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Wang WenbinPicha: picture-alliance/dpa/AP/L. Zheng

Mahusiano  baina ya  Marekani  na  serikali  ya  kikomunist  mjini Beijing  yalianza  kudhoofika  katika  miaka  ya  1970, wakati mahusiano  ya  China  na Urusi  ya  Umoja wa  Kisovieti yalipoporomoka na  kiongozi  mkuu  Mao Zedong alipohitaji  nguvu mbadala  kwa  jirani  yake  huyo  ambaye  ni  mwenye nguvu.

Kiongozi  mpya , Deng Xiaoping, alifanya  ziara  nchini  Marekani mwaka  1979  baada  ya  kuanzishwa  mahusiano  ya  kidiplomasia, akipiga  picha na  kutabasamu  huku  akivalia  kofia  maarufu inayovaliwa  na  wachunga  ng'ombe mjini  Houston. Ubalozi  ambao unafungwa mjini  humo  ulifunguliwa  baadaye  mwaka  huo huo. Ulikuwa  ubalozi  wa  kwanza  wa  China  nchini  Marekani.

USA Houston | Chinesische Konsulat
Huu ndio ubalozi mdogo wa Marekani mjini HoustonPicha: Getty Images/AFP/M. Felix

Wizara ya mambo  ya  kigeni  ya  China  ilisema jana  kuwa  hotuba aliyotoa  waziri  wa  mambo ya kigeni  Mike Pompeo  kuhusu  China haikutilia  maanani uhalisia na  ilijaa tu chuki  za  kinadharia.

Wang Wenbin , msemaji wa  wizara  ya mambo ya  kigeni aliwaambia  waandishi  habari  mjini  Beijing  kuwa  China inaitaka Marekani  kutupilia  mbali , "fikira  za  vita  baridi.