1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

China: Watoto ni uwekezaji muhimu katika kuimarisha uchumi

12 Desemba 2023

Taasisi inayoshughulikia masuala ya sera nchini China imesema watoto ni uwekezaji muhimu kwa uchumi wa China ili kuchochea na kukuza matumizi ya ndani ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4a47r
China | watoto na wazazi wakiwa katika michezo na watoto
Watoto wakiwa katika mafunzo ya michozoPicha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Taasisi hiyo metoa tamko baada ya China kwa mara ya kwanza katika muda wa miongo sita, kutoa data inayoonyesha kupungua kwa idadi ya watu. 

China, taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani imen'gan'gana kuuimarisha uchumi wake baada ya janga la COVID 19, na hatua yoyote ya kupungua kwa nguvu kazi na mahitaji ya ndani inaweza kuwa na athari mbaya kiuchumi. 

Soma pia:China yaikosowa sera ya biashara ya nje ya Ulaya

Serikali ilitangaza mikakati kadhaa kusaidiakupunguza ghara ya ulezi wa watotokatika miaka ya hivi karibuni, lakini sera nyingi hazijatekelezwa kutokana na ukosefu wa ufadhili wa kutosha.