1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China: Tuko tayari kuharibu hatua za kuipa Taiwan uhuru

16 Mei 2023

Jeshi la China limesema liko tayari kusambaratisha kwa uthabiti aina yoyote ya uhuru wa Taiwan, wakati Marekani ikijiandaa kuharakisha uuzaji wa silaha za kujihami na msaada mwingine wa kijeshi kwa kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4RSGL
China Außenminister Qin Gang
Picha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Kanali Tan Kefei amesema ongezeko la hivi karibuni la mahusiano ya kijeshi kati ya Washington na Taipei, ni hatua mbaya na hatarishi huku akiarifu kuwa Jeshi la Ukombozi la Umma wa China linaendelea kujiimarisha ili kukabiliana na uingiliaji wa kigeni na kwamba itatetea uhuru na mipaka ya nchi hiyo.

China inakichukulia kisiwa cha Taiwan chenye wakazi milioni 23 kama sehemu ya himaya yake na imekuwa ikiweka wazi uwezekano wa kutumia nguvu ili kudumisha udhibiti huo.