1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China na Urusi zaanza luteka ya pamoja ya kijeshi

17 Julai 2024

China na Urusi zimeanza luteka za kijeshi za majini katika Bahari ya China Kusini, katika hatua za kuimarisha uhusiano wa kijeshi na kibiashara kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4iPIo
China na Urusi zinafanya luteka ya pamoja
China na Urusi zaanza luteka za majini katika Bahari ya Kusini ya ChinaPicha: Iranian Army Office/ZUMA/picture alliance

Gazeti la serikali ya China la Global Times, limesema China na Urusi zitapeleka angalau meli tatu kila moja kwenye mazoezi hayo ya siku tatu, likinukuu kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa watu wa China.

Akizungumza na shirika la habari la kitaifa la China  CCTV, Wang Guangzheng afisa wa Jeshi la Wanamaji amesema doria za pamoja kati ya China na Urusi zimekuza ushirikiano wa kina na wa vitendo kati ya hizo mbili. 

China na Urusi zafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi

Luteka hizo zitajumuisha mafunzo ya mazoezi ya silaha za moto za majini, upelelezi na onyo la mapema, utafutaji na uokoaji, na ulinzi wa anga. Hata hivyo haikubainishwa ni wapi kwenye bahari hiyo inayogombaniwa mazoezi hayo yanafanyika.