1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

China na Urusi waikosoa Marekani katika mkutano wa kijeshi

30 Oktoba 2023

Wakuu wa jeshi wa China na Urusi wameikosoa Marekani siku ya Jumatatu katika mkutano wa usalama mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4YBfu
Maafisa wa gwaride la heshima wakiwa katika eneo la kongamano la Xiangshan mjini Beijing Oktoba 29, 2023. China na Marekani zaonekana kuanzisha tena mazungumzo kati ya majeshi yao.
Maafisa wa gwaride la heshima wakiwa katika eneo la kongamano la Xiangshan mjini Beijing Oktoba 29, 2023. China na Marekani zaonekana kuanzisha tena mazungumzo kati ya majeshi yao.Picha: Ng Han Guan/AP Photo/picture alliance

Hayo yamejiri licha ya kamanda wa cheo cha juu cha pili katika jeshi la China kuahidi kuimarisha mahusiano ya ulinzi na Marekani.

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amezionya nchi za Magharibi kwamba kuhusika kwake katika vita vya Ukraine kutasababisha hatari kubwa.

Naye Zhang Youxia ambaye ni naibu mwenyekiti wa Rais Xi Jinping katika Tume Kuu ya Kijeshi ya China ameikosoa Marekani na marafiki zake akidai baadhi ya nchi zinajaribu kuiendea kinyume serikali ya China.

Mkutano wa kijeshi wa Beijing Xianshan ambao ndio mkutano mkubwa zaidi wa China wa kuonyesha diplomasia yake ya kijeshi, ulianza jana bila uwepo wa waziri wa ulinzi wa China ambaye kawaida ndiye mwandalizi.

Mkutano huo ulijumuisha ujumbe wa Marekani licha ya mivutano iliyoko baina ya nchi hizo mbili.