1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Ufaransa wavijadili vita vya Israel- Hamas

20 Novemba 2023

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, wamejadiliana kuwa njia ya simu kuhusu vita ya Hamas na Israel na wote wamekubaliana kuepuka mgogoro wa kibinaadamu.

https://p.dw.com/p/4ZEfY
Diplomasia |  Xi Jinping na Emmanuel Macron
Diplomasia | Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ng Han Guan/AP/picture alliance

Kulingana na televisheni ya taifa ya China, CCTV, viongozi hao wawili wanaamini kipaumbele katika mgogoro huu ni kuepuka kuifanya hali kuwa mbaya zaidi kati ya Paelestina na Israel, na hasa kuepuka mgogoro mbaya zaidi wa kibinaadamu. 

Mazungumzi hayo ya simu yanajiri siku kadhaa kabla ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Catherine Colonna, na yanafanyika pia wakati ujumbe wa wanadiplomasia wakuukutoka Mamlaka ya Palestina, Indonesia, Misri, Saudi Arabia na Jordan wakikutana mjini Beijing kwa mazungumzo ya kuzuwia kutanuka kwa mgogoro wa Gaza.

Soma pia:China yatoa mwito kuzuwia kueneo mgogoro wa kibinadamu Gaza

Kulingana na CCTV, Xi na Macron wamekubaliana kuendelea na mawasiliano ya kimataifa na kikanda yanayowahusu na kuchangia upatikanajaji wa amani ya dunia na uthabiti.

CCTV imesema suluhisho la mataifa mawili kwa mzozo wa Israel na Palestina ni muelekeo muhimuwa kuutatua mgogoro unaotokea mara kwa mara kati ya pande hizo mbili.