1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Japan zathibitisha uhusiano wa kimkakati

17 Novemba 2023

Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wametangaza kujitolea kwao kukuza mahusiano yenye manufaa kwa pande zote mbili.

https://p.dw.com/p/4Z3Ub
USA | APEC  | San Francisco
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akiwa na rais wa China Xi Jinping Picha: Kyodo News via AP/picture alliance

Wamesema hayo wakati wa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana mwaka huu, ishara kwamba mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi barani Asia yanajaribu kuboresha uhusiano wao wenye matatizo.

Rais Xi alimwambia Kishida kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia maslahi ya pamoja na zithibitishe uhusiano wao wa kimkakati kwa manufaa ya pande zote mbili.

Xi Jinping na Fumio Kishida walifanya mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa kilele wa APEC, mjini San Francisco, nchini Marekani

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alisema alimwelezea Rais Xi Jinping wasiwasi wake mkubwa kuhusu shughuli za kijeshi za China karibu na Japan, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wake na Urusi.

Walisema hayo wakati wa mkutano wao wa pembezoni mwa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).