1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China: Meli ya kivita ya Marekani imevuka mipaka yake

23 Machi 2023

Jeshi la China limesema limeifuatilia na kulazimika kuifurusha katika maeneo ya mbali meli ya kivita ya Marekani ambayo imeingia kinyume cha sheria katika eneo la Bahari ya China Kusini.

https://p.dw.com/p/4P6zw
USS Nimitz Drill Südchinesisches Meer
Picha: ABACA/picture alliance

Taarifa ya jeshi la China imesema meli ya Marekani yenye mfumo wa kuharibu makombora aina ya USS Millus iliyoingia katika eneo la bahari la mipaka ya China inadhoofisha amani na utulivu katika njia ya maji yenye shughuli nyingi.

Lakini kwa upande wake jeshi la wanamaji la Marekani limetoa kauli ya kupinga taarifa ya jeshi la China kwa kusema meli hiyo imekuwa ikifanya opereshini za kawaida katika eneo la Bahari ya China Kusini na haikufurushwa.