1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China kuwekeza bilioni 100 kwenye miundombinu, biashara

18 Oktoba 2023

China itawekeza kiwango kipya cha zaidi ya dola bilioni 100 kwa mradi wake mkubwa wa ujenzi wa miundombinu na biashara.

https://p.dw.com/p/4XfiP
China | Seidenstraßengipfel
Rais Xi Jinping wa China akihutubia mkutano wa kilele wa mradi wa "Belt and Road."Picha: Edgar Su /REUTERS

Hayo yamsemwa na Rais Xi Jinping wa China hivi leo kwenye mkutano wa kilele unaoadhimisha miaka kumi tangu mradi huo ulipoanza.

Xi ametangaza kuwa wakopeshaji wakuu wa mradi huo, Benki ya Maendeleo ya China na benki inayotoa mitaji kwa ajili ya usafirishaji na uagizaji bidhaa nje na ndani ya nchi zitatoa mikopo ya ziada ya thamani ya dola bilioni 100.

Soma zaidi: Mkutano wa miundombinu waanza leo China

Mkutano wa wiki hii unaohudhriwa na wawakilishi kutoka nchi 130, ni wa tatu mkubwa wa kilele wa aina yake kuandaliwa na China tangu mradi wa ujenzi wa miundombinu na barabara ulipozinduliwa mnamo 2013.