1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China: Helikopta ya kijeshi ya Canada ilikiuka sheria

Angela Mdungu
4 Novemba 2023

Wizara ya Ulinzi ya China imesema kuwa, helikopta ya jeshi la Canada ilikiuka sheria ya nchi hiyo na ya Kimataifa kwa kuingia katika eneo la Bahari ya Kusini mwa China.

https://p.dw.com/p/4YP8P
Meli ya kijeshi ya China ikilinda doria Bahari ya Kusini mwa China
Meli ya kijeshi ya China ikilinda doria Bahari ya Kusini mwa ChinaPicha: Ted Aljibe/AFP

Msemaji wa wizara hiyo ameeleza kuwa kitendo hicho cha Canada, ni cha uovu na uchochezi na kwamba kinaweka rehani uhuru na usalama wa Beijing.

Soma zaidi: China, Ufilipino zagongana Bahari ya Kusini

Jana Ijumaa, Waziri wa Ulinzi wa Canada alizituhumu ndege za kivita za China kwa kuibughudhi helikopta yake katika eneo la kimataifa katika bahari ya Kusini mwa China mwishoni mwa juma lililopita, hali iliyohatarisha maisha ya waliokuwemo ndani yake. Akijibu tuhuma hizo, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China amesema hatua zilizochukuliwa na ndege za kivita za Beijing zilikuwa za kitaalamu na zilizingatia kanuni.