1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cheptegei kutafuta changamoto mpya kwenye marathon sasa

21 Agosti 2023

Joshua Cheptegei wa Uganda aliendelea kuzitawala mbio za mita elfu 10 baada ya kushinda dhahabu kwa dakika 27:51.42 mbele ya Mkenya Daniel Simiu Ebenyo aliyeandikisha muda wa dakika 27:52.60.

https://p.dw.com/p/4VPWM
Joshua Cheptegei kutoka Uganda
Joshua Cheptegei akishinda mbio za mita 10,000Picha: Petr David Josek/AP

Muethiopia Selemon Barega alimaliza katika nafasi ya tatu huko Budapest na kushinda medali ya shaba. Cheptegei sasa anatazamia kuchukua mkondo mwengine katika taaluma yake ya riadha.

"Labda wakati umewadia sasa nigeukie marathon. Kwasababu imekuwa safari njema ila kumekuwa na changamoto pia hasa kupata majeraha na baadae viwango kurudi chini. Ila yote tisa, nafurahia kushinda kwa kuwa hilo ndilo nililoliwaza," alisema Cheptegei.

Chanzo: DPAE/APE/Reuters