1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chauvin aomba kufunguliwa upya kesi ya mauaji ya Floyd

5 Mei 2021

Afisa wa zamani wa polisi mjini Minneapolis Marekani Derek Chauvin amemuomba jaji kuifungua upya kesi dhidi yake, akidai alinyimwa haki baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya bila kukusidia ya George Floyd.

https://p.dw.com/p/3sysV
Murder trial of former Minneapolis police officer Derek Chauvin
Picha: via REUTERS

Wakili Eric Nelson amesema mteja wake alinyimwa hakikatika kesi hiyo kwa sababu ilirushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, makosa ya kisheria na "shinikizo lenye msingi wa ubaguzi wa rangi" kwa baraza la wazee wa mahakama.

Waendesha mashitaka bado hawajawasilisha jibu dhidi ya hoja hizo.

Chauvin alishitakiwa kwa mauaji baada ya kuikandamiza shingo ya Floyd kwa goti huku akiwa amefungwa pingu, kwa zaidi ya dakika 9 mnamo Mei 25, 2020.