1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EMA: Chanjo za Covid-19 zaathiri hedhi kwa kina mama

29 Oktoba 2022

Wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya Ulaya (EMA) wameonya kuwa baadhi ya chanjo za Covid 19 zinaweza kusababisha kina mama kutokwa na damu nyingi za hedhi.

https://p.dw.com/p/4Ip7S
Impfstofffläschen von Moderna und Biontech
Picha: Bildagentur-online/Ohde/picture alliance

Wataalamu hao wametaka ugunduzi huo uongezwe katika orodha ya uwezekano wa athari inayoweza kutokea. Taarifa ya shirika hilo limetaja chanzo za Pfizer na Moderna, kuwa zimeonesha athari hizo na hasa katika chanjo ya pili au zile za nyongeza.

Kwa mujimbu ya mamlaka hiyo hatua ya hedhi ambayo inafanyika kwa kuongezeka kiwango cha utokaji damu au kufanyika kwa muda mrefu kinaathiri ustawi wa afya. "Hali hiyo imebainika katika chunguzi kadhaa za kitabibu." EMA ilisema.

Athari za kutokwa damu nyingi kunahusiana na chanjo

Katika hitimisho lake mamlka hiyo imesema "angalau kumekuwa na uwezekano kwamba kiwango kikubwa cha kutokwa na damu za hedhi ni athari inayohusishwa na aina hizo za chanjo."

Msemaji wa Moderna amesema kampuni yake ina taarifa za ripoti ambazo zinahusisha chanjio ya "dysmenorrhea" au maumivu yenye kuhusiana na kipindi cha hedhi. Lakini hata hivyo bado hawajagundua athari zenye kuhusiana na chanjo ya Moderna, Spikevax. Kwa upande mwingine kampuni ya BioNTech yenye kutengeneza chanjo ya Pfizer haikuweza kupatikana mara moja kueleza kuhusu ripoti hiyo.

Afya ya uzazi kwa kina mama bado salama

Frankreich Lyon | Coronavirus Impfstation
Muuguzi akimpatia chanjo muhudumiwaPicha: JEFF PACHOUD/AFP

Hata hivyo pia mamlaka EMA  imesema katika ripoti ya uchunguzi wake hakuna ushahidi wa wazi uanonesha matatizo ya hedhi yanayowapata baadhi ya kina mama yana athari yoyote katika suala la afya ya uzazi na uzazi wao.

Kikosi kazi cha dharura cha mamlaka hiyo kimesema chanjo za mRNA hazisababishi matatizo ya ujauzito mama wajawazito au watoto wao. Matukio ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi yamekuwa yakifanyiwa uchunguzi katika ngazi ya kitaifa na Ulaya kwa ujumla wake tangu ripoti za kwanza kuonekana kati ya wanawake waliochanjwa.

Soma zaidi:WHO: Maambukizi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu yaongezeka duniani

Matatizo ya hedhi kwa wakina mama yanaweza kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali zenye msingi wa kiafya, msongo wa mawazo na uchovu. Mamlaka za afya zimetoa zingatia baada ya ugunduzi kuonesha visa hivyo imeripotiwa baada ya kutokea mikasa ya maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Chanzo: RTR