Mbali ya vyombo vya habari na taasisi za elimu, lugha ya Kiswahili hukuzwa pia na waandishi wa riwaya na kazi nyengine za kifasihi. Katika Kiswahili Kina Wenyewe leo, Mohammed Khelef anazungumza na Enock Maregesi, mwandishi wa riwaya ya Kolonia Santita, iliyoshinda nafasi ya pili kwenye Tuzo ya Fasihi ya Kiswahili ya Mabati-Cornell mwaka 2015.