1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA wasusia uchaguzi wa Muhambwe

Sudi Mnette1 Aprili 2021

Chama kikuu cha Upinzani Tanzania-CHADEMA kimesema hakitoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma kwa madai ya kukosekana haki. Jimbo la Muhambwe limekuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia baada ya kupata ajali ya gari mapema Februari. Sudi Mnette alizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Benson Kigaila kuhusiana na hatua hiyo.

https://p.dw.com/p/3rVPY