1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chadema:Utafiti unaomuweka Magufuli kifua mbele, propaganda

1 Oktoba 2020

Chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema kinapuuzia matokeo ya utafiti wa taasisi ya Trends Dynamiques Consulting yanayoonesha asilimia 79 ya wapiga kura wakisema, watamchagua John Magufuli kama rais.

https://p.dw.com/p/3jI0u
Tansania Wahlen 2020 | Tundu Lissu
Picha: AFP

Chadema kinasema hizo ni propaganda za CCM katika kuwaanda wapiga kura kisaikolojia.

Chadema imesema hayo ikiwa ni siku moja tangu kutolewa kwa matokeo ya utafiti huo ambao unaonesha mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, atapigiwa kura kwa asilimia 19, kwa upande wa Tanzania bara na asilimia 28 kwa upande wa Zanzibar na kuutafrsiri kuwa huo ni mpango mwingine wa CCM katika kufanya hujuma za kuiba kura za wananchi.

Baadhi ya tafiti zinaonyesha Tundu Lissu atapigiwa kura na zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura

Akizungumza na DW Rodrick Rutembeka katibu mkuu baraza la wazee chadema amesema, wanapuuzia utafiti huo kwani ni sehemu ya propaganda ya chama tawala CCM katika kuhalalisha kumuweka mamlakani mgombea wao Rais John Magufuli ambae anawania muhula wa pili wa kuliongoza taifa hilo la Afrika mashartiki linaloingia katika uchaguzi wake wa sita tangu kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi 1992.

Tansania Tundu Lissu Präsidentschaftskandidat
Mgombea wa Chadema Tundu LissuPicha: DW/S. Khamis

Aidha ameongeza kuwa, hata chama chake tayari kimekwisha fuatilia tafiti kadhaaa zilizofanywa na watu binafsi na kuonesha kuwa bwana Tundu Lisu mgombea wa chama hicho kikuu cha upinzani atapigiwa kura kwa asilimia zaidi ya themanini, lakini hawakuziweka hadharani kwa kuwa wanasubiri maamuzi ya kidemocrasia yanayotokana na kura za raia.

Kwa upande wa chama tawala CCM kimesema kinaridhia matokeo hayo sababu mgombea wake Rais John Magufuli anakubalika na wananchi kutokana na yale aliyoyafanya katika awamu ya kwanza ya uongozi wake, hivyo hawana sababu ya kununua utafiti ili kuwaaminisha wapiga kura.

Waliohojia na Trends Dynamiques Consulting wasema watamchagua Magufuli kama rais

Mwalimu Raymond Mangwala ni katibu mkuu wa umoja wa vijana CCM taifa ameiambia DW kuwa katika utafiti walioufanya kama vijana wa chama hicho umeonesha Rais Magufuli atashinda kwa zaidi ya asilimia 90. alisisitiza.

Afrika Tansania Mosambik SADC  John Magufuli
Mgombea urais wa CCM John Pombe MagufuliPicha: DW/D. Khamis

Kwa mujibu wa waliohojiwa na taasisi ya Trends Dynamiques Consulting walisema watamchagua Rais Magufuli kutokana na uwezo wa kulinda maslahi ya taifa na ujenzi wa miundombinu, huku waliosema watamchagua Tundu lisu sababui zao zikiwa ni ujasiri wake na kuhitaji mabadiliko kutokana na CCM kukaa mamalakani kipindi kirefu.