Chad yamshutumu Macron kwa kuwadharau Waafrika
7 Januari 2025Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Abderamane Koulamallah amesema kwenye taarifa iliyotolewa hapo jana kwamba tabia ya Macron inaashiria jeuri kwa Afrika na Waafrika.
Tamko lililosomwa kwenye televisheni ya taifa hilo la Afrika ya Kati imesema kwamba viongozi wa Kifaransa wanapaswa kujifundisha kuwa na heshima kwa Waafrika.
Soma zaidi: Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kunawatia wasiwasi Wachad
Koulamallah amesema kwenye tamko hilo kwamba badala yake Ufaransa inapaswa kukumbuka jukumu kubwa la Afrika na Chad kwenye ukombozi wa Ufaransa wakati wa vita viwili vikuu vya dunia, jambo ambalo halijawahi hata mara kutambuliwa na Ufaransa.
Vile vile waziri huyo alisema mchango wa Ufaransa kwa Chad daima umekuwa ukijikita kwenye maeneo ya maslahi ya kimkakati ya mkoloni huyo wa zamani na sio kwa maendeleo ya kudumu ya watu wa Chad.