1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChad

Chad yafungua ubalozi wa kwanza nchini Israel

2 Februari 2023

Rais Mahamat Idris Deby Itno wa Chad amefungua ubalozi wa kwanza wa taifa lake nchini Israel, miaka minne baada ya mataifa hayo kufufua uhusiano kufuatia miongo kadhaa ya mzozo.

https://p.dw.com/p/4N26b
Tschad Junta Mahamat Idriss Deby Itno
Picha: Denis Sassou Gueipeur/AFP

Rais Mahamat Idris Deby Itno wa Chad amefungua ubalozi wa kwanza wa taifa lake nchini Israel, miaka minne baada ya mataifa hayo kufufua uhusiano kufuatia miongo kadhaa ya mzozo.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, imesema ufunguaji wa ubalozi huo katika mji wa Ramat Gan karibu na Tel Aviv ulikuwa wa kihistoria.

Israel iliitambua Chad wakati ilipotangaza uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1960 na kufikia 1962, ilikuwa imefungua ubalozi wake mjini N'djamena.

Uhusiano kati ya Israel an Chad ulivunjika mwaka 1972, kufuatia shinikizo kutoka mataifa ya Kiislamu ya Afrika, lakini ulirejea baada ya ziara ya Netanyahu nchini Chad mwaka 2019.