1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CENI yatangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa wabunge

Jean Noël Ba-Mweze
22 Januari 2024

Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) ilitangaza matokeo ya muda ya uchaguzi wa wabunge wa mikoa usiku wa Jumapili ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu kura kupigwa.

https://p.dw.com/p/4bYPQ
DR Kongo Kinshasa 2023 | CENI | Didi Manara
Naibu Mwenyekiti wa CENI, Didi Manara.Picha: Saleh Mwanamilongo/DW

Watu 688 ndio walichaguliwa kuwa wabunge wa mikoa kati ya 780 nchini humo.

Idadi itaongezwa baada ya baadhi ya changamoto kutatuliwa katika baadhi ya maeneo.

Vyama vya UDPS cha Rais Felix Tshisekedi pamoja na Union Sacrée, unaojumuisha vyama vya vinavyotawala ndivyo vimepata wabunge wengi wa mikoa kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa wabunge wa kitaifa. 

Matokeo yaliyotangazwa hayahusu baadhi ya maeneo kama Budjala mkoani Ubangi Kusini, Bomongo na Makanza mkoani Equateur ambako uchunguzi bado unaendelea kutokana na hitilafu za uchaguzi. 

Maeneo mengine ni Masimanimba mkoani Kwilu na Yakoma huko Ubangi Kaskazini ambapo kura zilifutwa kutokana na udanganyifu na maeneo ya Masisi na Rustshuru ambako uchaguzi haukufanyika kutokana na ukosefu wa usalama.