1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDC Afrika yaitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma

14 Agosti 2024

Kituo cha kudhibiti na kuzuia magongwa barani Afrika, (Africa CDC), kimeutangaza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani kuwa hali ya dharura kwa afya ya umma.

https://p.dw.com/p/4jRhg
Homa ya nyani
CDC Afrika yaitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya ummaPicha: CDC/Getty Images

Kituo hicho kimetoa tangazo hilo baada ya kuongezeka idadi ya watu walioambukizwa maradhi hayo yanayosababishwa na kirusi kinachoitwa MPOX.

Mlipuko wa ugonjwa huo umeyakumba mataifa kadhaa ya Afrika, na hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako ugonjwa huo uligundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1970.

Africa CDC yaitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma

Kulingana na takwimu za CDC hadi kufikia mapema mwezi huu watu 38,465 walikuwa wameambukizwa  kirusi cha mpox na wengine 1,456 wamekufa barani Afrika tangu Januari 2022.

CDC imetoa tamko kabla ya kufanyika mkutano wa dharura wa shirika la afya duniani, WHO, hapo kesho kuamua iwapo shirika hilo litangaze dharura ya kimataifa kutokana na mlipuko huo.