1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS: Chaves asema kiongozi wa Cuba amepata nafuu

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCA1

Rais Hugo Chaves wa Venezuela amesema kwamba kiongozi wa Cuba Fidel Castro anaendelea kuimarika katika hali yake ya afya na kwamba hadi sasa ameweza kutekeleza majukumu yake kadhaa ya urais.

Castro alifanyiwa upasuaji miezi minane iliyopita katika utumbo wake na kutokea wakati huo nduguye Raul alishikilia madaraka ya nchi kwa muda.