1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANCUN:Kimbunga Wilma sasa kinaelekea Cuba na Florida

23 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEPE

Kimbunga Wilma kimeuwa watu 3 na kimesababisha uharibifu mkubwa katika rasi ya Yucatan nchini Mexico.Mjumbe wa serikali amesema uharibifu wa aina hiyo haujawahi kutokea.Mji wa Cancun unaotembelewa sana na watalii umefurika kufuatia mvua kubwa zilizonyesha.Watalii kwa maelfu wamehamishwa na kupelekwa katika maeneo yenye usalama fulani.Watabari wa hali ya hewa wamesema kimbunga Wilma sasa kinaelekea Cuba na Florida.Nchini Marekani,wakaazi wa Florida Keys wanalazimishwa kuhama,kwa sababu Kimbunga Wilma kinatazamiwa kuwasili eneo hilo siku ya Jumatatu.Safari hii Marekani inatahadhari zaidi katika matayarisho yake kuhusu Kimbunga Wilma,baada ya kulaumiwa sana kuwa haikujitayarisha vya kutosha pale Kimbunga Katrina kilipovuma mwaka huu na kuteketeza eneo zima kusini mwa nchi,ikiwa ni pamoja na mji wa New Orleans.Wilma ni kimbunga cha 12 kuvuma kwenye eneo la Atlantic msimu huu wa vimbunga.Hiyo ni idadi kubwa kabisa ya vimbunga vilivyovuma eneo hilo tangu mwaka 1969.