1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANBERRA: Australia inakataa kuitikia wito wa waasi

7 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFFp

Australia imekariri kuwa haitotekeleza madai yaliotolewa na waasi waliomzuia mateka raia mmoja wa Australia nchini Iraq.Waasi hao wanaitaka Australia iyaondoshe majeshi yake kutoka Iraq.Msimamo mkakamavu wa Australia umetangazwa wakati stesheni ya televisheni ya Al Jazeera imeonyesha kanda mpya video.Kanda hiyo yamuonyesha mkandarasi wa Australia Douglas Wood akiketi,huku bunduki mbili zikilengwa kwenye kicha chake.Australia ina kama wanajeshi 550 nchini Iraq,na wengine 350 wanatazamiwa kupelekwa hivi karibuni.Utekajinyara huu na mashambulio yanayozidi nchini Iraq,yanahatarisha uwezo wa serikali mpya kuwashinda waasi.Hadi watu 200 wamefariki katika mfululizo wa mashambulio ya waasi tangu kuundwa kwa serikali ya Iraq wiki iliyopita.