1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiCanada

Canada yamtia hatiani mtu mmoja kwa mauaji ya kukusudia

17 Novemba 2023

Mahakama moja ya Canada imempata na hatia mwanamume wa umri wa miaka 22 kwa mauaji ya watu wanne wa familia moja ya Kiislamu katika shambulio lililofanyika mwaka wa 2021

https://p.dw.com/p/4YzLe
Mahakama kuu ya Canada
Mahakama kuu ya CanadaPicha: Adrian Wyld/empics/picture alliance

Nathaniel Veltman alitiwa hatiani kwa makosa manne ya mauaji ya kukusudia na shtaka moja la kujaribu kuua.

Veltman aligonga wanafamilia hao kwa kutumia lori lake la kubebea mizigo mnamo Juni 2021 huko Ontario.

Upande wa mashtaka wadai shambulio hilo ni la kutia hofu waislamu

Upande wa mashtaka ulidai kuwa shambulio hilo lilitaka kuwatisha au kuwatia hofu Waislamu, likichochewa na itikadi kali ya ukuu ya wazungu.

Shambulizi hilo lilikuwa baya zaidi dhidi ya waislamu nchini Canada tangu shambulio la bunduki katika msikiti wa mmoja huko Quebec City mwaka 2017 lililosababisha vifo vya watu sita.