1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CALEDONIA FARM:Sio ya kuridhisha hali asema mjumbe wa Umoja wa Mataifa

1 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEyJ

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Anna Tibaijuka aliyeitembelea Zibwabwe kujiona hali ilivyo amekiri hii leo kwamba hali sio nzuri kwenye kambi wanamoishi watu waliovunjiwa nyumba zao na serikali ya rais Robert Mugabe.

Bi Tibaijuka amesema hatua zinapasa kuchukuliwa kuyaimarisha maisha ya watu hao,baada ya kutembelea kambi ya Caledonia iliyoko kilomita 25 mashariki mwa mji wa Harare.

Takriban watu elfu 4500 kwenye kambi hiyo wanaishi kwenye nyumba zilizotengenezwa kwa makaratasi ya plastiki kwa mujibu wa bibi Tibaijuka baada ya nyumba zao kubomolewa wiki iliyopita.

Serikali ya Mugabe ilizibomoa nyumba za maelfu ya watu kwa kile ilichokiita operesheni ya kusafisha mazingira na kumaliza uhalifu nchini Zimbabwe.