1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF yatangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia 2026

20 Mei 2023

Shirikisho la soka Afrika CAF, limetangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia la mwaka 2026. Katika mfumo huo mpya, mataifa 54 wanachama wa CAF yatagawanywa katika makundi tisa.

https://p.dw.com/p/4RbLO
Fußball 2023 Africa Cup of Nations | Viertelfinale, Marokko v Algerien
Picha: Shaun Roy/Sports/empics/picture alliance

Kila mshindi wa kundi atajihakikishia nafasi katika fainali za kwanza zinazoshirikisha timu 48, ambazo zitaandaliwa na Marekani, Canada na Mexico. Kombe la Dunia la mwaka 2022 nchini Qatar lilishirikisha nchi 32.

Taarifa iliyotolewa baada ya kikao cha kamati kuu ya CAF nchini Algeria imesema kuwa droo ya mchujo itafanyika jijini Cotonou mnamo Julai 12 nchini Benin. Wakati huo huo, CAF pia imetangaza kuwa droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya 2023 nchini Ivory Coast itafanyika Oktoba 12.