1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush asema silaha kwa Saudi Arabia ni ruhsa

15 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CphN

RIYADH:

Rais George W.Bush wa Marekani ambae sasa yuko Saudi Arabia kwa ziara rasmi, amesema kuwa nchi yake itaendelea mbele na mpango wake wa kuiuzia Saudia Arabia silaha.

Mpango huo, wenye utatanishi na kugharimu mabilioni kadhaa ya dola, umezusha wasiwasi nchini Israel pamoja na baadhi ya washirika wake katika eneo hilo.Saudi Arabia ndio kituo cha mwisho cha safari yake katika mashariki ya kati.Rais Bush anatumia ziara yake hii ya mashariki ya kati kujaribu kutafuta kuungwa mkono katika shabaha yake ya kupata mkataba wa amani kati ya Wapalestina na Israel kabla ya kumalizika muhula wake katika kipindi kijacho cha mwaka.